News
NTSA yarudisha huduma za utoaji wa nambari za usajili wa magari nchini.
Mwenyekiti wa mamlaka ya kitaifa ya uchukuzi na usalama barabarani nchini, NTSA Khateeb Mwashetani amesema wamerudisha huduma za utoaji wa nambari za usajili wa magari baada ya upungufu uliokithiri kwa miezi kadhaa.
Mwashetani amesema NTSA imeanza kupokea nambari za usajili wa magari na kuzisambaza kwa wale ambao wanatuma maombi ya kupata nambari hizo.
Aidha, Mwashetani amesema juhudi zimewekwa kuhakikisha mchakato huo wa kutengeneza na kutuoa nambari hizo zinatekelezwa bila changamoto zozote.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa NTSA George Njau amewahakikishia wafanyabiashara wa magari na wananchi kuwa changamoto za masuala ya ugavi zilizopelekea tatizo hilo zimeangaziwa ipasavyo.
Kurejeshwa kwa huduma za utoaji wa nambari za usajili wa magari ni afueni kwa wamiliki wengi wa magari nchini ambao walikuwa na changamoto hiyo.