Sports

Zaidi ya Wachezaji 200 Waungana Railways Golf Club kwa Mashindano ya KCB East Africa Golf Tour 2025

Published

on

Uwanja wa Gofu wa Railways (Par 72) unatarajiwa kuwapokea zaidi ya wachezaji 200 wa gofu kwa awamu ya kumi na nane ya Mashindano ya KCB East Africa Golf Tour 2025 siku ya Jumamosi.

Baada ya tamasha la kuvutia lililofanyika wikendi iliyopita kule Sigona, mashindano haya ya kanda yanatarajiwa kuanza mapema saa 12:30 asubuhi kwa raundi ya kwanza, kabla ya raundi ya mchana itakayoanza saa sita kamili mchana.

Akizungumza kabla ya mashindano haya, Nahodha wa Railways Golf Club, John Kamenyi, alisema wanatarajia idadi kubwa ya washiriki Jumamosi. “Mfululizo huu umekuwa muhimu sana katika kuwapa maelfu ya wapenzi wa gofu nafasi ya kuboresha ujuzi wao na pia kufurahia mchezo huu. Tumefanya kazi kubwa kuhakikisha uwanja uko katika hali bora, kwa hivyo wachezaji watarajie burudani ya hali ya juu,” alisema Kamenyi.

Hadi sasa, Mashindano ya KCB East Africa Golf Tour 2025 yamehusisha zaidi ya wachezaji 2,000 kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na zaidi ya watoto 1,000 kupitia kliniki za golf zinazofanyika sambamba na mashindano haya.

Hapa nchini Kenya, mashindano haya tayari yamefanyika katika kaunti 10 ikiwemo Nairobi, Nakuru, Kisumu, Laikipia, Nandi, Mombasa, Kisii, Kiambu, Machakos na Kericho.

Katika nje ya nchi, mashindano hayo yamefanyika Uganda na Burundi, huku Tanzania na Rwanda zikitarajiwa kuwa wenyeji kabla ya fainali kuu kufanyika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version