Sports

Yoane Wissa Afuta Picha Zote Zinazomhusisha na Brenford Mitandaoni

Published

on

Mshambulizi wa kilabu ya Brenford Yoane Wissa amefuta picha zake zote zinazomhusisha na kilabu yake hiyo.

Mshambuliaji huyo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, aliondolewa kwenye kikosi cha Brentford kilichopoteza 3-1 dhidi ya Nottingham Forest Jumapili, huku akisisitiza kutaka kujiunga na Newcastle.

Newcastle tayari imetuma angalau ofa moja iliyokataliwa na Brentford majira haya ya kiangazi. BBC Sport iliripoti awali kwamba Wissa alirudi nyumbani mapema kutoka kambi ya maandalizi ya msimu nchini Ureno, na kutishia kutoichezea wala kuendelea na mazoezi ikiwa uhamisho wake kwenda St James’ Park hautakubaliwa.

Baadaye kulikuwa na ishara za maridhiano kidogo, jambo lililomfanya kurejea kambini kwa mazoezi na kikosi cha kwanza, ingawa aliweka wazi kuwa anataka kujiunga na Newcastle.

Inadaiwa kuwa wakati huo, Wissa aliamini Brentford wangeruhusu uhamisho wake mara tu wangepata mchezaji mbadala. Hata hivyo, licha ya Brentford kukamilisha usajili wa Dango Ouattara kutoka Bournemouth, bado wanachelewa kutoa ruhusa huku kukiwa na madai kwamba sasa wanamthamini Wissa kwa kiwango cha juu kuliko bei yao ya awali ya pauni milioni 40.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version