Sports
Waziri Wa Usalama Murkomen Asema Tuko Tayari Chan
Waziri wa Usalama wa ndaani Kipchumba Murkomen amesema kwamba Taifa la Kenya liko tayari kwa kipute cha CHAN mwezi ujao.
Akizungumza na wanahabari hapo jana Murkomen amesema miondo misingi ya usafiri na usalama iko tayari kwa sasa wakiwa tayari kulinda usalama wa timu zote na mashabiki nje na ndaani ya uwanja.
Murkomen pia amerai mashabiki kufika uwanjani kumiminika katika viwanja mbalimbali kupiga jeki kikosi cha Stars kuweza kufanya kweli kama mchezaji wa 12.
“Viwanja vya viko tayari hata zile za mazoezi kwa ajili ya Taji hili Spesheli,tuko tayari kulinda timu zote na wachezaji pamoja na mashabiki watakao kuja nchini kushabikia timu zao nchini,Pia Nichukue fursa kurai Wakenya kujitokeza kwa wingi kuwa mtu wa 12 kushabikia vijana wa nyumbani Harambee Stars.
Kwa mujibu wa Murkomen viwanja vyote vitakavyotumika vina usalama mkubwa na wanamikakati ya kuzuia tukio lolote ambalo linaweza tokea kwenye kipute hicho kwani wamejipanga vyema kabisaa.
Kombe hilo linangoa nanga Agosti 2 uwanjani Benjamin Mkapa nchini Tanzania.