News

Watu wawili wahofiwa kuangamia baharini Lamu

Published

on

Watu wawili wanahofiwa kufariki baada ya boti walimokuwa wakisafiria kuelekea eneo la Shanga Kisiwani Patekaunti ya Lamu kuzama bahari hindi kwa siku ya tatu leo.

Ibrahim Chole na Hassan Njoroge wanasemekana walikuwa wakitoka kisiwani Amu kuelekea Shanga kupeleka mafuta kusaidia boti lengine ambalo lilikuwa limeishiwa na mafuta kabla ya kutoweka.

Taarifa ilisema boti yao baadaye ilipatikana eneo la Kizingitini kisiwani Pate huku wawili haowakikosekana.

Aidha vitengo mbali mbali vya ukombozi vikiongozwa na msimamizi wa kitengo cha Coast Guard Lamu Juma Difwiri walisema serikali ya kaunti, wananchi pamoja na Redcross wanaendesha oparesheni kuwasaka wawili hao ambao hawajulikani walipo.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version