News
Mahakama ya Shanzu kubaini hatma ya Washukiwa wa wizi, Mtwapa
Washukiwa 7 waliokamatwa katika eneo la Mtwapa kaunti Kilifi kwa tuhuma za wizi kwenye magari watafahamu hatma yao siku ya Ijumaa 13 mwezi huu iwapo wataachiliwa kwa dhaman au la.
Washukiwa hao Edwin Kyalo Mulandi, Nicholus Mungaro Kitumbo maarufu Papa, Erick Kabue Maranga maarufu Wachira, Ali Said Nassir, Fred Mungoma Mwanjira, Fredrick Kalungo Konde na Akasha Hassan Akasha walifikishwa katika Mahakama ya Shanzu kaunti ya Mombasa ambako walikanusha mashtaka dhidi yao.
Aidha, upande wa mashtaka uliwasilisha ombi la kutaka saba hao kunyimwa dhamana ikizingatiwa kwamba ni miongoni mwa wahalifu sugu ambao walikuwa wakitafutwa na asasi za usalama, baadhi yao wakiwa na rekodi za kesi Mahakamani.
Saba hao walikamatwa baada ya kuhusishwa na visa vya wizi viliyoripotiwa katika vituo mbalimbali vya polisi ikiwemo Mtwapa kaunti ya Kilifi, Changamwe, Nyali, Tononoka, Makupa na Central, kaunti ya Mombasa, kituo cha Embakasi jijini Nairobi na Dar es Salaam nchini Tanzania.
Wakati wa kukamatwa 7 hao, polisi pia walifanikiwa kunasa magari 8 na bidhaa mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 7.
Taarifa ya Mwanahabari wetu.