Sports
Vilabu Vya KCB Na GSU Mabingwa Taji La Kenya Cup
Kilabu ya wanabenki KCB ya wanawake ndiyo mabingwa wa Voliboli taji mpya la Kenya Cup fainali iliopigwa ugani Kasarani Indoor Arena wikendi hii.
Hii ni baada ya vipusa hao wa kocha Japheth Munala kuwashinda Kenya Pipeline kwa seti 3-0 za 25-16,25-19,25-22 katika fainali kali ilipigwa katika uga huo
Kwa mujibu wa kocha huyo ni kwamba haikua mechi rahisi kwao na mabingwa wa taji la ligi ya Voliboli nchini Kenya Pipeline ila walikua wamejipanga vizuri kwa mechi hiyo kuliko mechi yoyote ile.
“Tunaheshimu sana wapinzani wetu,ila niliambiwa wachezaji wangu wamejitoe zaidi kwani nilijua si mechi rahisi dhidi ya Pipeline kwani ni timu nzuri mno.”
Katika upande wa wanaume kilabu ya GSU ilinyuka WanaKDF seti 3-0 za 25-22,26-24,25-17 na kuibukia mabingwa wa kombe hilo.