News

UNICEF: Watoto milioni 138 wanashiriki ajira za utotoni

Published

on

Takriban watoto milioni 138 walishirikishwa katika ajira za watoto kote duniani mwaka 2024.

Kulingana na ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la umoja wa mataifa la watoto duniani, UNICEF na Shirika la kimataifa la ajira, ILO ilionyesha wazi kwamba watoto hao walikuwa wakinyanyaswa haki zao za kimsingi.

Idadi hiyo inajumuisha karibu watoto milioni 54 ambao walifanya ajira ambazo huenda zikaathiri afya na usalama wao.

Mkuu wa UNICEF, Christian Schneider alisema Ripoti hiyo pia ilisema visa vya ajira kwa watoto vinafanyika aghalabu katika Kilimo huku mataifa yaliyo chini ya Jangwa la Sahara yakiathirika pakubwa ambapo watoto milioni 87 waliathirika.

“Ripoti mpya ya ajira kwa watoto ilionyesha ukweli mchungu kwamba mamilioni ya watoto bado wananyimwa haki ya kusoma, kucheza na kuwa watoto, licha ya maendeleo yaliyopatikana,” alisema Schneider.

Idadi hiyo lakini ilionyesha kupungua kwa idadi ya watoto wanaoathirika kwani katika kipindi cha kati ya mwaka 2021-2024, idadi ya watoto walioshiriki ajira za utotoni ni 138 ikilinganishwa na mwaka 2016-2020 ambapo watoto milioni 160 waligundulika kufanya kazi.

Licha ya kupungua kwa idadi hiyo, lengo la kuangamiza ajira kwa watoto kufikia mwaka 2025 halitofikiwa kama ilivyoainishwa kwenye malengo ya ustawi ya Umoja wa Mataifa.

Ripoti hiyo ilitolewa kuelekea siku ya kimataifa ya kupinga ajira kwa watoto duniani itakayoadhimishwa siku ya Alhamis.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version