Business

Uhaba wa Samaki Wakumba Sekta ya Uvuvi Malindi

Published

on

Sekta ya uvuvi katika mji wa Malindi kaunti ya Kilifi, inaendelea kukumbwa na changamoto  kufuatia upepo mkali unaovuma baharini kwa kipindi cha wiki kadhaa sasa, hali inayosababisha uhaba mkubwa wa samaki sokoni na kuporomoka kwa mapato ya wavuvi.

Kwa mujibu wa Yunus Aboud Sahe, Mwenyekiti wa ufuo wa bahari katika eneo la Shella, upepo huo ulilazimu wavuvi wengi kusitisha shughuli zao za kila siku kutokana na hatari ya kuzama au kupata ajali baharini.

Sahe alisema kuwa hali hiyo imesababisha idadi kubwa ya wavuvi kukaa nyumbani, jambo ambalo linaathiri vibaya mapato yao na ustawi wa familia zao.

“Kwa sasa, hata wale wachache wanaothubutu kuingia baharini wanarejea na wastani wa kilo mbili pekee za samaki, licha ya kuhatarisha maisha yao. Hii ni hali ngumu kiuchumi na inahitaji suluhisho la haraka,” alisema Sahe.

Aidha, aliwasihi wavuvi hasa wanaovua katika maji ya kina kirefu kuwa waangalifu na kutoingia baharini wakati wa upepo mkali, bali wawe na subira hadi hali ya anga itakapokuwa salama.

Alisisitiza umuhimu wa kuzingatia tahadhari ili kuepuka majanga ambayo yamekuwa yakishuhudiwa mara kwa mara katika eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version