Sports

Tuko Tayari Kwa CHAN Asema Kocha Wa Angola-Pedro

Published

on

SIKU 9 KUNGOA NANGA KWA CHAN
ANGOLA-Mabingwa wa Taji La COSAFA.
Wanajiita The Black Antelopes kwa jina la utani ila bado hawajashinda kombe la CHAN katika historia yao.
Taifa hilo limeshiriki kombe hilo miaka minne ikiwa ni miaka ya  (2011, 2016, 2018, 2022) zote wakiambulia patupu.
Kocha mkuu wa timu hiyo ya taifa anaitwa Pedro Gonçalves ambaye ameongoza timu za taifa hilo kuanzia kwa vikosi chipukizi wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 taji la AFCON NA COSAFA ya chipukizi kabila ya kuongoza taifa hilo kushinda kombe la COSAFA wakishinda Afrika Kuisini magoli 3-0 kwenye fainali mwezi jana.
Akizungumza kabila ya timu hiyo kuwasili jijini Nairobi mwalimu huyo amesema lengo lao ni kuendeleza walipoachia ; “Tumefanya vizuri sana Cosafa na sasa lengo letu kushinda Chan pia nina kikosi ambacho kiko tayari na tutafanya kila kitu kuibuka washindi.”
Mwalimu huyo pia ameongoza taifa lake katika kombe la AFCON mwaka 2024 wakitolewa kwenye robo fainali nchini Ivory Coast.
The Sable Antelopes ilimaliza nafasi ya nne taji la Chan katika fainali ya mwaka 2011 nchini Sudan.
Badhi ya wachezaji wa kuangaziwa katika kikosi cha vijana hao ni pamoja na ;mshambulizi Jó Paciência wa kilabu ya Bravos do Maquis nchini humo mabeki Eddie Afonso na Hossi.
Mabingwa hao wa COSAFA wako kundi A pamoja na Kenya,Morocco,DR.Congo na Zambia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version