Winga Bukayo Saka aongeza mkataba mnono na Klabu yake ya Arsenal hadi mwaka 2031

Winga Bukayo Saka aongeza mkataba mnono na Klabu yake ya Arsenal hadi mwaka 2031
Winga machachari wa taifa la Uingereza Bukayo Saka ametia wino mkataba mpya wa miaka mitano na klabu yake ya Arsenal ya London Kaskazini.
Mkataba huo mpya unamfanya Saka kuwa mchezaji ghali kwa sasa katika klabu hiyo akiwa ataendelea kuhudumia wanabunduki hao hadi mwaka 2031.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 sasa atakua anapokea mshahara wa pauni laki tatu ÂŁ300,000 kwa wiki zaidi ya mchezaji yeyote katika kambi ya The Gunners.
Wachezaji wengine waliongeza mkataba wa muda mrefu na the Gunners ni pamoja na William Saliba, Gabriel Magalhaes, Ethan Nwaneri na Myles Lewis-Skelly.
Saka amefunga jumla ya magoli 57 ambayo ameyafunga akiwajibikia klabu ya Arsenal na timu ya taifa la England.