Waumini wa dini ya kikristo waadhimisha ibada ya majivu

Waumini wa dini ya kikristo waadhimisha ibada ya majivu

Waumini wa Kanisa Katoliki pamoja na waumini wengine wa dini ya kikristo wameungana kote ulimwenguni kuadhimisha ibada ya Misa ya Jumatano ya majivu ishara ya kuanza kwa kipindi cha mfungo wa siku 40 yani Kwaresma.

Padri wa Kanisa Katoliki la St. Patrick mjini Kilifi Henry Ndune alisema kwamba kipindi cha Kwaresma kina ashiria kujinyima kula na kunywa, kujitenga na maovu na dhani pamoja na ushawishi amba0 huenda ukamfanya mwanadamu kutokuwa karibu na mwenyezi Mungu.

Kulingana na Padre Ndune, kipindi cha Kwaresma hukamilika na maadhimisho ya siku ya Alhamis kuu ambapo kuhani huwaosha miguu wanaume 12 kama kumbukumba ambazo Yesu Kristo alifanya kabla ya kuhukumiwa na kufariki.

Siku ya Ijumaa kuu kabla ya ufufuko wa Yesu Kristo ambayo kuadhimishwa kabla ya sikukuu ya Pasaka, huashirikia ukumbusha wa mateso aliyopitia Yesu Kristo kabla ya kifo chake na baada ya siku tatu akafufuka kutoka kwa wafu kulingana na imani ya dini ya kikristo.

Padre Ndune, katika maelezo yake kuhusu kipindi cha Kwaresma alisema sio Kanisa Katoliki pekee linaloadhimisha mfungo wa siku 40,  lakini pia makanisa mengine kufanya hivyo yenye imani ya dini ya kikristo ikiwemo Kanisa Kianglikana.

Padre Ndune alieleza kuwa sababu ya wakristo kuadhimisha ibada ya majivu ni kuashiria unyenyekevu sawa na kukumbushwa kuhusu umuhimu wa kujitenga na ubinafsi.

Taarifa ya Hamis Kombe