Golikipa aliyeng’ara Kwenye Coco FM Supercup ajiunga na Sango Sportiff

Golikipa aliyeng’ara Kwenye Coco FM Supercup ajiunga na Sango Sportiff
Ni rasmi golikipa wa klabu ya Beach bay ya Magharini Khaki Nickson amejiunga na klabu ya Sango sportiff ya Tana River inayoshiriki ligi ya divisheni ya Kwanza nchini.
 Mchezaji huyo ni kipa hatari ambaye aliweza kuonyesha uhodari wake kwenye Mashindano ya #CocoFMSuperCup2025 makala ya kwanza ambapo alitajwa miongoni mwa magolikipa bora akifikisha Klabu hiyo katika hatua ya fainali ambapo walipoteza kupitia penalti mikononi mwa Mbungoni United.
Katika mechi ya hatua ya nusu fainali kipa huyo aliweza kupangua penalti 2 dhidi ya Matano mane wakati timu yake ikifuzu katika hatua ya fainali kwa kishindo.Khaki amekua na klabu hiyo kuanzia anamaliza shule ya upili na sasa analenga juu zaidi na klabu yake hiyo mpya.
Sasa anajiunga tena na wachezaji wenzake Fred na Ushindi ambao wote wamewahi kuitumikia Beachbay FC miaka za awali.