Klabu ya Tottemham imempiga kalamu kocha wake Thomas Frank

Klabu ya Tottemham imempiga kalamu kocha wake Thomas Frank

Klabu ya Tottenham Hotspur imemfuta kazi kocha Thomas Frank miezi nane tu baada ya kumteua kuwa kocha mkuu.

Kwenye taarifa iliyotolewa leo Jumatano Feb 11 ilieleza : “Klabu imechukua uamuzi wa kufanya mabadiliko katika nafasi ya Kocha Mkuu Thomas Frank.”
Katika siku za hivi karibuni kocha huyo Raia huyo wa Denmark amekuwa na shinikizo nyingi kufuatia matokeo mabaya yaliyoifanya Spurs kushuka hadi nafasi ya 16 kwenye Jadwali la Ligi Kuu ya Uingereza.
Kichapo Cha Tottenham Hotspur kutoka kwa Newcastle United nyumbani ulikuwa wa mwisho Kwa kocha huyo kusalia kuiongoza Tottenham.
Frank ameshinda mechi saba tu kati ya 26 za ligi na kupoteza 11, na timu hiyo kushika daraja ikiwa pointi tano pekee.
Aidha Spurs pia walibanduliwa kwenye Kombe la FA katika raundi ya tatu na Aston Villa , na katika hatua ya 16 bora ya Kombe la Carabao na Newcastle, ingawa walimaliza nafasi ya nne katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Spurs wamekusanya pointi mbili pekee katika mechi zao sita za mwisho za ligi chini ya kocha na Frank.