Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2027 itakayofanyika Kenya, Uganda na Tanzania inaweza kuahirishwa kutokana na Maandalizi ya kusua sua.

Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2027 itakayofanyika Kenya, Uganda na Tanzania inaweza kuahirishwa kutokana na Maandalizi ya kusua sua.
Kamati ya utendaji ya Shirikisho la soka Afrika (CAF) inatarajiwa kukutana jijini Dar es Salaam, Tanzania, Ijumaa ya leo Februari 13, 2026.
Inaelezwa kuwa tayari Tanzania na Uganda zimelipa Dola Milioni 30 kuandaa michuano hiyo, lakini Kenya bado haijalipa haki kamili.
Ikiwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika itaahirishwa, itasogezwa hadi 2028, kwani kuanzia hapo michuano hiyo itachezwa kila baada ya miaka minne badala ya kila baada ya miaka miwili.
Kikao cha Kamati ya utendaji ya CAF kinatarajiwa kuthibitisha kujiondoa kwa Morocco katika kuandaa kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake 2026 mwezi ujao, baada ya nafasi yake kuchukuliwa na Afrika Kusini.
Fainali za kombe la Mataifa ya Afrika 2027 zimepangwa kuanza Mei 19 hadi 18 Julai 2027.
Itafanyika katika viwanja 10, ambavyo ni uwanja wa Benjamin Mkapa, Uwanja wa Samia Suluhu Hassan, Uwanja wa Dodoma na uwanja wa Amaan nchini Tanzania, Uwanja wa michezo wa Talanta, kituo cha michezo cha kimataifa cha Moi, uwanja wa Taifa wa Nyayo, Uwanja wa Bukhungu na Kipchoge Keino nchini Kenya.
Nchini Uganda, itafanyika kwenye Uwanja wa Hoima City, Uwanja wa Akii Bua na Uwanja wa Taifa wa Mandela.