News

Serikali yatoa shilingi milioni 60 kwa waathiriwa wa mafuriko Tana River

Published

on

Serikali ya kitaifa imezindua mpango wa msaada wa shilingi milioni 60 kwa wakazi wa Tana River walioathiriwa na mafuriko ya kudumu.

Mpango huo ulizinduliwa na katibu mkuu wa mipango maalum Ismail Maalim na mwenzake wa maswala ya kuangazia ardhi kame- ASALS Kello Harsama siku ya jumatatu 16, juni 2025.

Akizungumza katika eneo la Majengo, Maalim alisisitiza umuhimu wa zoezi hilo akisema ni wajibu wa kikatiba kwa serikali kutoa msaada wa chakula kwa wananchi wake.

Maalim aliongeza kuwa zaidi ya wakenya milioni 2 watapokea msaada wa chakula kutoka kwa serikali.

Kwa upande wake, Harsama alisema serikali tayari imesambaza mabati kwa waathiriwa wa mafuriko katika kaunti hiyo wakiwemo watu 600 walioathirika na mafuriko katika eneo bunge la Galole.

Makatibu hao walizuru kaunti nzima wakisambaza chakula cha msaada, magodoro na blanketi kwa wakazi, wakiandama na mbunge wa Garsen Ali Wario, mbunge wa Galole Said Buya na Mbunge wa Bura Yakub Adow.

Taarifa na Joseph Jira.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version