News

Serikali yatenga shilingi milioni 250 kwa Walemavu.

Published

on

Serikali kupitia Wizara ya Leba na maslahi ya kijamii imetenga shilingi milioni 250 mwaka wa 2025 ili kuimarisha uwezeshaji wa watu wanaoishi na ulemavu nchini.

Katibu mkuu wa wizara hiyo Joseph Motari alitangaza kuwa ufadhili huo utasaidia masuala ya elimu, kuwawesha kiuchumi pamoja na teknolojia kwa jamii hiyo.

Motari alibainisha hayo wakati wa kikao cha 18 cha mkutano wa nchi wanachama wa mkataba wa haki za watu wenye ulemavu (CRPD) jijini New York nchini Marekani.

“Kenya inaongeza juhudi zake za kujumuisha uchumi kwa kutenga zaidi ya shilingi milioni 250 mwaka huu kupitia msaada wa elimu, uwezeshaji wa kiuchumi na msaada wa kiteknolojia”, Motari alisema.

Katibu huyo pia aliangazia utekelezaji wa mpangilio wa mkakati wa mwaka 2023-27 ambao unayapa kipaumbela masuala ya ufahamu, uwezeshaji wa kijamii na kiuchumi, vile vile ujumuishaji wa kidijitali kwa watu wanaoishi na ulemavu.

Kulingana na Motari, takribani makaazi elfu 63 yatanufaika na program za serikali za kusambaza pesa na upokezaji wa marupurupu ya kila mwezi ya shilingi elfu mbili.

Kati ya hao zaidi ya walengwa elfu 20 wanafadhiliwa chini ya mpango ujulikanao kama Autism and Developmental Disabilities programme.

Mwaka 2024, serikali ilisambaza takriban vifaa 4,200 vya usaidizi kwa jamii hiyo pamoja na kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 2,500 wanaoishi na ulemavu.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version