Business

CBK: Bei za bidhaa za chakula zaendelea kupanda

Published

on

Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Benki Kuu ya Kenya (CBK) katika sekta ya Kilimo umebainisha kuwa kuna ongezeko la bei ya bidhaa muhimu za chakula, ikiwemo Mahindi, Sukari, na Mafuta ya kupikia.

Ripoti hiyo ilionyesha kuwa mabadiliko haya ya bei yanachochewa na sababu mbalimbali za kitaifa na kimataifa, zenye athari kubwa kwa walaji wa kawaida na sekta ya biashara kwa ujumla.

Kwa mujibu wa CBK, bei ya Mahindi imekuwa ikiongezeka tangu wiki za mwisho za mwezi Mei.

Hali hii imepelekea ongezeko la bei ya paketi ya kilo 2 ya unga wa Mahindi kwa wastani wa shilingi 6, hatua ambayo wasagaji wa unga wa Mahindi wameitaja kuwa imesababishwa na uhaba wa Mahindi sokoni.

Kukabiliana na changamoto hiyo, Wizara ya Kilimo nchini imeingilia kati kwa kusambaza magunia laki mbili ya Mahindi kwa wasagaji mbalimbali kote nchini, ili kusaidia kudhibiti bei na kuhakikisha upatikanaji wa unga kwa wananchi kwa gharama nafuu zaidi.

Wakati huo huo, bei ya sukari na mafuta ya kupikia pia inatarajiwa kuendelea kupanda.

Ongezeko hili linahusishwa na mabadiliko ya bei katika masoko ya kimataifa, hasa kutokana na kupungua kwa uzalishaji katika baadhi ya nchi zinazouza bidhaa hizo kwa wingi, pamoja na gharama za usafirishaji zinazoendelea kuongezeka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version