Sports
PSG Imepunguza Ada ya Ununuzi wa Kipa Gianluigi Donnarumma
Kilabu ya PSG ya Ufaransa imeripotiwa kupunguza ada waliyotarajia kwa kipa wa Kiitaliano Gianluigi Donnarumma kufuatia nia kutoka kwa kilabu ya Manchester City.
Donnarumma, mwenye umri wa miaka 26, ameuhusishwa na Citizens, ambao wanatafuta kipa mpya iwapo Ederson ataondoka klabuni.
Kulingana na RMC Sport, mabingwa wa sasa wa Ligi ya Mabingwa wamepunguza bei yao kutoka pauni milioni 43 hadi kati ya pauni milioni 26 na 30, ikizingatiwa kuwa Donnarumma amebakisha mwaka mmoja pekee kwenye mkataba wake jijini Paris.
Hali hiyo imemfanya Luis Enrique kuachana na mchezaji muhimu wa kikosi chake kilichoshinda Ligi ya Mabingwa, na kumweka badala yake Lucas Chevalier.
Nguli wa taarifa za Uhamisho Fabrizio Romano pia ameripoti kuwa masharti binafsi yamekubaliwa kati ya Donnarumma na Manchester City, huku dili hilo likionekana kukaribia kukamilika.
Kuingia kwa Donnarumma kungehitaji kuzingatiwa kwa kuuzwa kipa namba moja wa muda mrefu wa Guardiola, Ederson. Mbrazil huyo, ambaye amechezea klabu hiyo tangu mwaka 2017, hakudumu kama chaguo la kwanza msimu uliopita, mara nyingi akibadilishana nafasi na Stefan Ortega.