News
Papa Francis Ameaga Dunia akiwa na Umri wa Miaka 88
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 88.
Uongozi wa Kanisa Katoliki umethibitisha kifo chake na kusema kwamba Papa Francis ameaga dunia asubuhi siku ya Jumatatu ya Pasaka Aprili 21 katika makaazi yake katika Casa Santa Marta, Vatican.
Kadinali Kevin Farrell, Camerlengo Vatican amesema Kanisa Katoliki liko na huzuni kubwa kwa kumpoteza kiongozi huyo.
Kadinali Farrell amesisitiza umuhimu wa waumuni wa Kanisa Katoliki kuzingatia mafunzo ya Papa Francis ya utumishi kwa ajili ya Kanisa na kuthamini maisha ya utume.
Kadinali Farrell amehimiza ulimwengu kuzingatia uamunifu, ujasiri na upendo hasa kwa ajili ya maskini na wale waliotengwa jinsi Papa Francis alivyokuwa akihimiza ulimwengu.
Papa Francis alionekana mara ya mwisho akiwasalimia waumini wa Kanisa Katoliki wakati wa Ibada ya Misa ya Jumapili ya Pasaka katika Kanisa la St Peters Square mjini Rome na kuwahimiza waumini kuthamini ufufuko wa Yesu Kristu wakati wanapoadhimisha Pasaka.
Papa Franics hata hivyo alikuwa akiugua ugonjwa wa amonia ya mapafu na kulazwa kwa zaidi ya wiki tatu hospitalini na baadaye akarejea katika makaazi yake baada ya kupata nafuu kabla ya kuaga dunia siku ya Juamtatu, Aprili 21.