Rais William Ruto na Gavana wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja wametia saini makubaliano ya kihistoria ya ushirikiano kwa ajili ya kuboresha jiji la Nairobi.
Mkataba huo uliyo upo rasmi kwenye kifungu cha 6 cha sheria ya maeneo ya miji, unaweka mfumo rasmi wa ushirikiano kati ya serikali hizo mbili.
Makubaliano hayo yalisainiwa na Mkuu wa mawaziri nchini Musalia Mudavadi kwa niaba ya serikali ya kitaifa na Gavana Sakaja kwa niaba ya Serikali ya kaunti ya Nairobi.
Rais Ruto, aliyeshuhudia zoezi hilo, ameweka wazi kwamba mpango huo hauashirii kuchukuliwa kwa majukumu ya kaunti, akisisitiza kuwa mpangilio huo ni wa ushirikiano na kifedha pekee.
Hafla hiyo hata hivyo iliandaliwa katika Ikulu ya Nairobi siku ya Jumanne, Februari 17, 2026
Taarifa ya Joseph Jira
