Mahakama Kuu imesimamisha kwa muda agizo la kuondolewa afisini kwa Katibu Mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna.
Katika uamuzi uliotolewa Alhamis 12 2026, Mahakama ilitoa amri ya muda ya kuzuia utekelezaji wa mchakato wa kumng’oa Sifuna katika wadhifa wake kama Katibu mkuu wa chama cha ODM, hadi kesi iliyowasilishwa Mahakamani itakaposkizwa na kuamuliwa.
Hatua hiyo inafuatia mzozo wa ndani wa chama kuhusu uongozi wa nafasi hiyo, ambapo kulikuwa na jaribio la kumtimua mamlakani.
Kutokana na uamuzi huo, Sifuna ataendelea kuhudumu kama Katibu Mkuu wa ODM hadi pale mahakama itakapotoa mwelekeo au uamuzi wa mwisho kuhusu suala hilo.
