Serikali kuu inalenga kupanua mradi wa Galana Kulalu

Serikali kuu inalenga kupanua mradi wa Galana Kulalu

Serikali ya kitaifa imepanga kupanua mradi wa kilimo cha chakula wa Galana Kulalu kama sehemu ya juhudi za kuimarisha usalama wa chakula nchini ili kusaidia zaidi ya kaunti 23 zinazokabiliwa na uhaba wa chakula.

Waziri wa maji nchini Mhandisi Eric Mugaa, alisema serikali inalenga kuongeza eneo la Kilimo kwa ekari elfu 10 ili kufikia jumla ya ekari elfu 20 zinazolimwa kwa sasa na kampuni ya Selu.

Aidha alihoji kwamba kufikia mwezi Mei, mwekezaji huyo atakuwa tayari amelima takriban ekari elfu 10, akibainisha kwamba Mamlaka ya kitaifa ya unyunyizi (NIA), tayari imesaini mkataba na mkandarasi wa ujenzi wa bwawa la Galana.

“Tumelima zaidi ya ekari elfu mbili na tuko katika ile safari ya kuhakikisha kwamba itakapofika mwezi wa tano katikati yule mwekezaji wa kibinafsi atakuwa amelima ekari zaidi ya elfu”, alisema Eric.

Kwa upande wake, Katibu katika Idara ya Unyunyizaji, Ephantus Kimotho, amesema serikali imeweka mikakati madhubuti ya kuongeza uzalishaji wa chakula kwa wingi.

Taarifa ya Mwanahabari wetu