Sifuna atimuliwa kutoka wadhifa wake wa Katibu mkuu wa ODM

Sifuna atimuliwa kutoka wadhifa wake wa Katibu mkuu wa ODM

Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna ametimuliwa kutoka wadhifa wake kama Katibu mkuu wa Chama cha ODM na nafasi yake kuchukuliwa na Catherine Omanyo.

Uamuzi huu umeafikiwa katika kikao maluum cha Kamati kuu ya Chama cha ODM kilichofanyika Februari 11 mjini Mombasa na kuongozwa na Kinara wa Chama hicho Dkt Oburu Oginga.

Hatua hiyo ambayo haikutarajiwa hivi karibuni ilizua gumzo na hisia mseto na kuzidisha mpasuko na joto la siasa ndani ya Chama cha ODM.

Ni dhahiri kwamba Edwin Sifuna sasa ataongoza mrengo wenye siasa kali ndani ya Chama hicho cha ODM kinachoungwa mkono na
Ruth Odinga,‎Winnie Odinga, ‎Babu Owino, ‎Caleb Amisi, ‎James Orengo, ‎Majimbo Kalasinga na ‎Richard Onyonka.

Mzozo ndani ya Chama Cha ODM uliibuka baada ya Kifo cha mwasisi na Kinara wa Chama hicho Marehemu Raila Amollo Odinga kuhusu tofauti za mstakabali wa Chama.

Kinara wa sasa Oburu Odinga na wandani wake wanasititiza Chama kusalia kwenye mpango wa serikali jumuishi chini ya Rais William Ruto kwa kuheshimu wosia wa Marehemu Raila huku kambi inayoongozwa na Edwin Sifuna na Babu Owino ikipinga kauli hiyo.

Mrengo wa Kinara wa Chama hicho Oburu Odinga umekuwa ukiendelea kampeni ya Linda Ground huku Edwin Sifuna na James Orengo wakianzasha vuguvugu la ODM Lina Mwananchi na mkutano wa hivi punde  ukiandaliwa Busia.