News
Mzugha, awahimiza vijana kaunti ya Taita taveta kuzingatia elimu
Mwakilishi wa wadi ya Mbololo kaunti ya Taita taveta Lawrence Mzugha ametoa wito kwa vijana katika eneo hilo kuzingatia elimu.
Kulingana na Mzugha kuna nafasi nyingi za ajira ikiwemo uendeshaji bodaboda, magari miongoni mwa fursa nyingine za kujikimu kimaisha ambazo zinahitaji ujuzi.
Aidha, Mzugha aliahidi kuwaunga mkono vijana wa wadi yake wanaonuia kupata ujuzi kupitia ufadhili unaotolewa na serikali ikiwemo basari na michango mingine katika jamii hasa ule wa kufadhili elimu.
“Kwa uwezo wa Mungu kuna baadhi ya vitu ambavyo nimefanya, maana kwa elimu muswada wa kwanza kuingia bungeni kuhusu elimu, mimi ndio nilipeleke’’, alisema Mzugha.
Mzugha alisema fomu za basari katika wadi hiyo ya Mbololo zinapatikana kwa mtandao.
Taarifa ya Janet Mumbi