News
Misri kuanzisha kituo cha usafirishaji baharini jijini Mombasa.
Serikali ya Misri imepanga kuanzisha kituo cha mwaswala ya maji na usafirishaji baharini jijini Mombasa kama sehemu ya ushirikiano katika ya kenya na Misri.
Tangazo hilo limetolewa na balozi wa Misri nchini Kenya Wael Nasreldin Attiya wakati wa kikao kati yake na uongozi wa halmashauri ya bandari nchini Kenya- KPA, ukiongozwa na mkurugenzi mkuu Nahodha William Ruto.
Balozi Attiya alipongeza uekezaji wa Kenya katika miundo mbinu hasa katika bandari ya Mombasa, akisema umeimarisha ufanisa na kuifanya Kenya kama kitovu muhimu cha usafirishaji ukanda wa afrika mashariki.
Kwa upande wake Nahodha William Ruto alikaribisha waekezaji kutoka Misri na kuwahimiza kutumia fursa zinazotokana na maboresho ya miundo mbinu nchini Kenya huku akiahidi ushirikiano wa dhati kutoka halmashauri ya KPA.
Taarifa ya Joseph Jira