News

Migos: Serikali imeanzisha mipango ya kuimarisha idara ya ukaguzi wa shule

Published

on

Waziri wa Elimu nchini Julius Migos Ogamba, alisema serikali imeanzisha mipango ya kuimarisha idara ya ukaguzi wa shule ili kuhakikisha fedha zinazotengewa taasisi za elimu zinatumika ipasavyo.

Akizungumza jijini Mombasa, Waziri Migos alieleza kwamba sekta ya elimu imetengewa mgao mkubwa katika bajeti ya kitaifa ya mwaka wa fedha wa 2025/2026 na kwamba ni lazima fedha hizo zitumike ipasavyo.

Waziri huyo vile vile alidokeza kwamba serikali inapanga kuajiri walimu elfu 24 katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha ujao ili kupunguza tatizo la uhaba wa walimu mashuleni.

“Kama serikali tumepanga kuajiri walimu wengine elfu 24 ili kukabiliana na changamoto za ukosefu wa walimu shuleni na kusaidia wanafunzi wetu kuendelea na masomo na pesa tumetenga ya kutosha”, alisema Migos.

Wakati uo huo, aliunga mkono uamuzi wa Mahakama kuu kupiga marufuku shule kutoza ada za ziada, akisema walimu wakuu wanaowatoza wazazi fedha zaidi kinyume na sheria, watakumbana na mkono wa sheria.

Taarifa ya Mwanahabari wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version