Business

Mgomo wa Tuktuk Tezo waathiri biashara

Published

on

Shughuli za kibiashara katika soko la Tezo kaunti ya kilifi ziliathirika jumatatu ya Julai, 21, 2025 kufuatia mgomo wa wahudumu wa tuktuk.

Kulingana na wafanyibiashara katika soko hilo, wengi wao wanategemea huduma za tuktuk kusafirisha bidhaa zao hadi katika soko hilo.

Wakizungumza na cocofm wafanyibiashara hao waliongeza kuwa wateja wengi pia hutegemea usafiri wa tuktuk kufika sokoni humo, na kufuatia mgomo huo wengi walikosa kufika hali ambayo iliwasababishia hasara kubwa.

Aidha waliitaka sekta ya tuktuk kurejesha huduma hizo ili kuwapa afueni wafanyibiashara ikizingatiwa kuwa wanategemea biashara kujikimu kimaisha.

Mgomo huo wa wahudumu wa tuktuk uliwapa wadumu wa bodaboda mjini kilifi kaunti ya kilifi fursa ya kuvuna zaidi kimapato.

Kulingana na wanaboda wa eneo la Tezo mgomo wa wahudumu wa tuktuk uliwapelekea fursa ya kuongeza nauli kutokana na idadi kubwa ya wateja.

Kutoka eneo la Tezo hadi Chumani wahudumu hao walibeba abiria mmoja kwa shilingi 200 tofauti na shilingi 100 ya hapo awali.

Wahudumu wa tuktuk waligoma kutokana na kupanda kwa bei za mafuta aina ya petroli na dizeli, hali ambayo wanasema inasawababishia harasa kubwa.

Taarifa ya Pauline Mwango

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version