News
Mbarire, Awaonya Viongozi wa Kenya Kwanza
Mvutano wa kisiasa umeanza kushuhudiwa ndani ya Chama tawala cha UDA baada ya baadhi ya viongozi wa chama hicho kutofautiana kisiasa huku wengine wakilalamikia kudharauliwa.
Mwenyekiti wa kitaifa wa chama hicho Cecily Mbarire amewaonya baadhi ya viongozi wa Kenya kwanza dhidi ya kuingilia shughuli za viongozi wengine na badala yake kuhakikisha wanawajibikia majukumu yao.
Mbarire ambaye pia ni Gavana wa kaunti ya Embu amesema baadhi ya viongozi wa Chama hicho wamekuwa wakimkosea heshima kama Mwenyekiti wa kitaifa wa UDA na kupanga mikutano ya kisiasa ndani ya kaunti yake ya Embu bila ya kumhusisha.
Aidha amewataka viongozi hao kutotumia nafasi zao vibaya kutokana na kuwa karibu na rais akisema iwapo kuna masuala ibuka basi itakuwa vyema iwapo viongozi wote wakuu chamani watahusishwa na kutatua changamoto hizo.