Sports
Martin Zubimendi Mali Ya Arsenal
Kilabu ya Arsenal imetangaza rasmi usajili wa kiungo wa Uhispania Martin Zubimendi kwa dau la pauni milioni 51 ambayo inakisiwa kufika pauni milioni 60 badaye.
Mchezaji huyo wa Real Sociadad ametia wino mkataba wa miaka mitano baada ya kupasi vipimo vya kimatibabu ugani Emirates.
The Gunners kwa sasa wako kwenye mazungumzo na mshambulizi wa sporting lisbon victor gyokeres ikiwa sporting wako karibu kukubali dili hiyo kwa pauni milioni 67.
Zubimendi ni mshindi huyo wa kombe la Euro na Uhispania amechezea kilabu yake mechi 236 na taifa lake mechi 19 .