News
Mahakama Yawapa Matumaini Wanahabari wa VOA
Ni afuani kwa zaidi ya wafanyikazi 1,300 wakiwemo Wanahabari kutoka Kenya wa kituo cha habari za kimataifa cha Sauti ya Amerika VOA baada ya Mahahama kubatilisha uamuzi wa Rais Donald Trump wa kukifunga kituo hicho.
Mahakama kuu ya Washington imeagiza kituo hicho cha habari cha VOA cha miaka mingi kuendelea na majukumu yake ya kikazi ya kuhabarisha ulimwengu matukio mbalimbali yanayojiri na serikali ya Trump imeagiza kutoingilia utendakazi wa VOA.
Mahakama hiyo imeutaka utawala wa rais Trump kuwarejesha kazini wafanyikazi wote waliopewa likizo ya lazima na kuwasilisha ripoti kuhusu kandarasi zao.
Mkurugenzi wa VOA Michael Abramowitz amedai kufurahishwa na uamuzi huo wa Mahakama akisema utawala wa rais Trump ulikuwa umewafungia nje wafanyikazi wengi pamoja na kudhohofisha usimamizi wa kituo hicho cha habari.
Itakumbukwa kwamba mapema mwaka huu rais Trump alitia saini agizo la kufungwa kwa kituo hicho cha kimataifa cha habari kwa madai ya kupunguza gharama ya matumizi ya serikali yake.