News
Maandamano ya makumbusho ya Juni 25
Wakenya wa tabaka mbalimbali wamejitokeza katikati mwa miji mkuu nchini Kenya ikiwemo Nairobi, Mombasa, Nakuru, miongoni mwa miji mingine kuadhimisha makumbusho ya Juni 25.
Maandamano hayo ya kuwakumbuka vijana wa kizazi cha Gen z walioaga dunia kwenye maandamano ya kupinga mswada wa fedha wa mwaka 2025 yanaendelea katikati mwa miji hiyo.
Katika jiji la Mombasa maandamano hayo yanaendelea kwa amani huku Wanaharakati wa kijamii na vijana wa Gen Z wakiandamana na maafisa wa polisi kwa njia ya amani na usalama wa hali ya juu.
Jijini Nairobi na Nakuru hali ni tofauti kwani waandamanaji hao walianza kurushia mawe na maafisa wa polisi kinyume na jinsi maandamano hayo yalivyotarajiwa huku maafisa wa polisi wakitumia vitoa machozi ili kuwatawanya waandamanaji.
Katika jiji la Nakuru hali ni sawa na Nairobi kwani mshikeshike wa maafisa wa polisi wa kukabiliana na ghasia na waandamanaji wanakabiliana vilivyo huku barabara zote na shughuli za kibiashara zikifungwa.
Katika jiji la Kisumu hali ni tofuati kwani hakuna maandamano anayoendelea katika jiji hilo huku shughuli za kawaida za kibiashara na uchukuzi zikiendelea kwa utaratibu.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi