News

Lagat, kuhojiwa na IPOA kuhusu kifo cha Ojwang

Published

on

Naibu Inspekta jenerali wa Polisi Eluid Lagat, anatarajiwa kufika mbele ya Mamlaka ya kuchunguza utendakazi wa maafisa wa polisi nchini IPOA kuhojiwa siku ya Alhamis Juni, 19.

Lagat ambaye alijiondoa ofisini kwa kuhusishwa na mauaji ya mwanablogu Albert Ojwang anatarajiwa kuweka wazi anachokifahamu kuhusu mauaji ya Ojwang na kwa nini alitoa idhini ya kukamatwa na kutendewa unyama huo.

Akizungumza na Wanahabari, Mwenyekiti wa Mamlaka ya IPOA Issack Hassan alisema yeyote atakaypatikana na hatia katika kesi hiyo ni lazima atachukuliwa hatua kali za kisheria ili haki kwa muathiriwa ipatikane.

Hassan aliwataka wakenya kuwa na subra wakati maafisa wa upelelezi wa IPOA wanapotekeleza majukumu yao kwani Lagat ameagiza kufika mbele ya Mamlaka hiyo ili kuhojiwa na kuandikia taarifa kuhusiana na mauaji ya Ojwang.

“Tumemuagiza Lagat kufika mbele ya maafisa wetu wa uchunguzi wa IPOA kuhojiwa na kuandikisha taarifa kuhusu kesi ya mauaji ya Ojwang kwa hivyo wakenya wawe na subra na yeyote atakayepatikana na tabia atakabiliwa kisheria”, alisema Hassan.

Wakati huo huo Mahakama iliagiza kwamba Afisa mkuu wa Polisi anayesimamia kituo cha polisi cha Central jijini Nairobi Samson Talam ataendelea kuzuiliwa kwa siku 14 zaidi.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version