Sports
Kilabu Ya Arsenal Yapata Pigo baada ya Mshambulizi Kai Hervertz Kupata Jeraha la Goti
Mshambulizi wa Arsenal Kai Havertz anaripotiwa kupata tena pigo la majeraha baada ya kuumia goti, jambo lililomfanya kukosa mazoezi ya Arsenal kwenye uwanja wa Emirates mapema leo.
mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, alikosa nusu ya pili ya msimu uliopita baada ya kupata jeraha kubwa la misuli ya paja wakati wa kambi ya mazoezi ya kati ya msimu ya Arsenal huko Dubai.
Kwa mujibu wa The Athletic, jeraha la mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani sasa linailazimisha Arsenal kurudi sokoni kusaka mshambuliaji mpya.
Mshambulizi mpya Viktor Gyokeres kwa sasa ndiye mshambuliaji pekee aliye timamu kiafya anayepatikana kwa Arteta, huku Gabriel Jesus akiwa bado nje kwa muda mrefu baada ya kujeruhiwa anterior cruciate ligament (ACL) mnamo Januari.