News

Jamii ya Wapokomo yalalamikia uongozi wa Mombasa

Published

on

Jamii ya wapokomo wanaoishi kaunti ya Mombasa wamelalamikia kutengwa na serikali ya kaunti hiyo kwa kile wanachodai kuwa ni ubaguzi wa kikabila.

Wakiongozwa na mwenyekiti wao, Abdhalla Bakar, walisema licha ya kuishi Mombasa kwa muda mrefu na kuwa wapiga kura katika kaunti hiyo, jamii hiyo haijawahi kuhusishwa ipasavyo katika mipango ya maendeleo, wala kuteuliwa kwenye nafasi muhimu za kiutawala.

Kwa mujibu wa Bakar, jamii ya Wapokomo imeendelea kusahaulika katika upangaji wa bajeti, utoaji wa zabuni, ajira, na huduma muhimu za kijamii.

“Serikali zote za Mombasa huwa hazitutambui, dhana ni kwamba sisi huenda kupiga kura kwetu lakini sisi zaidi ya kura elfu 20 huwa tunazipiga hapa Mombasa, lakini ukienda kwa serikali ya kaunti hatuna mfanyakazi yeyote kutoka kwa jamii ya Chanamaro, ukienda kwa wanasiasa hatuna hata diwani”, alisema Bakar.

Kwa upande wake mbunge wa eneo bunge la Galole kaunti ya Tana River Said Hiribae alieleza masikitiko yake kuhusu suala hilo, akiitaka serikali ya kaunti ya Mombasa kuhakikisha inajumuisha jamii zote bila ubaguzi.

“Hapa Mombasa kabila hizi kunazaidi ya kura elfu 20, na hizo kura elfu 20 zote hazijawasaidia Chanamaro, kwa sababu ukiangalia kabila zingine pengine wanaweza kupata wacha uwakilishi wadi, hata ubunge pia wangepata”, alisema Hiribae.

Taarifa ya Mwanahabari wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version