International News

Israel na Iran zakubaliana kusitisha mashambulizi

Published

on

Warning
Warning
Warning
Warning

Warning.

Makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Iran yameanza kutekelezwa huku nchi hizo mbili zikithibitisha tangazo la Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu hatua hiyo.

Muda mfupi baada ya tangazo la Trump, taifa la Israel lilisema limeafikia malengo yake na ikathibitisha kwamba imesitisha mashambulizi, hatua iliyotafsiriwa kama mwisho wa vita vya siku 12 kati ya Israel na Iran.

Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya nje wa Iran, Abbas Araghchi, ilikanusha kuwepo kwa makubaliano yoyote ya kusitisha mashambulizi, akisema kwamba Iran haina nia ya kuendeleza mashambulizi, lakini bado haijakubali rasmi kusitisha mapigano.

Licha ya kauli za kusitishwa kwa mashambulizi ya makombora kati ya nchi hizo mbili, Jeshi la Ulinzi la Israel limeripoti mashambulizi mapya yaliyotokea kutoka upande wa Iran.

Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz alisema Iran ilikiuka usitishaji wa mapigano kwa kurusha makombora, akisema huenda jeshi la Israel likaanza tena kuishambulia Iran.

Iran ilikanusha habari kwamba imefanya mashambulizi ya makombora kuelekea Israel baada ya nchi hizo mbili kukubali kusitisha mapigano.

Mataifa mbalimbali ulimwenguni yamepongeza hatua ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Iran, huku taifa la China likizitaka nchini hizo mbili kutafuta suluhisho la kisiasa kwa mzozo kati yao.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version