News
Idara ya Usalama Yalaumiwa kwa Kukosa Kuhamia Mfumo wa Kidijitali
Idara ya Usalama nchini imelaumiwa kwa kushindwa kuzihamisha huduma zake hadi katika mfumo wa kidijitali hali ambayo imerudisha nyuma juhudi za kutafuta usaidizi wa kiusalama.
Kulingana na Wanaharakati wa kijamii, licha ya taifa kupiga hatua katika kuhakikisha haki inapatikana kwa washukiwa na wale wanaofika Mahakamani bado idara hiyo imesalia nyuma kiteknolojia.
Wanaharakati hao wakiongozwa na Victor Kaudo, wamelaumu mfumo wa zamani unaotumika na maafisa wa usalama katika kunakili na kuweka rekodi za kesi mbalimbali zinazowasilishwa katika vituo vya polisi, wakidai kwamba mfumo huo unachelewesha kesi Mahakamani.
“The next Place ambayo tunahitaji zaidi iende digital ni National Police service ili zile faili pale ziwe zinafanywa haraka haraka ndio tukienda pale katika Gender base tuache kuwa frastrated and alot of paper work. Wakifanya kazi zote kuwa katika mtandao tutakuwa tunafanya kazi zetu kwa urahisi”, alisema Kaudo.
Hata hivyo mwaka wa 2019, Idara ya usalama nchini ilianzisha mchakato wa kuweka rekodi za kesi wanazopokea katika mfumo wa kidijitali lakini mpango huo ilikosa kufaulu na kuwarejesha katika mfumo wa zamani wa kutumia vitabu kunakili kesi.