Sports

Duplantis Tayari Kwa Mashindano Ya Dunia Tokyo,Japan

Published

on

Mshikilizi wa rekodi kuruka juu (pole vault) kutumia kijiti Armand ‘Mondo’ Duplantis ametabiri mashindano ya dunia “yatakuwa ya kipekee mno” jijini Tokyo, ambako alinyakua medali yake ya kwanza ya Olimpiki katika Michezo ya Majira ya Kiangazi iliyocheleweshwa na janga la Covid, lakini akasisitiza kuwa takwimu kwake si jambo la maana.

Mchezaji huyo mzaliwa wa Marekani mwenye uraia wa Uswidi amekuwa kwenye kiwango cha juu, akiweka rekodi yake ya dunia ya 13 kwa kuruka mita 6.29 mjini Budapest siku ya Jumanne, hatua inayozidi kuthibitisha nafasi yake kama mmoja wa wanariadha bora zaidi katika historia ya riadha.

Hata hivyo, Duplantis huepuka mbwembwe ambazo mara nyingi huonyeshwa na wakimbiaji wa masafa mafupi, akisisitiza kuwa hahangaiki na mchezo wa nambari.
“Ninachojali ni kuhakikisha kwamba kila kitu kidogo kimekamilika, kila undani umekaa sawa, na kwamba niko tayari kwa wakati muhimu zaidi,” Duplantis alisema Alhamisi kabla ya mashindano ya Diamond League huko Silesia, Poland.

“Kuna heshima kubwa,” alikiri kuhusu kuweka rekodi nyingi za dunia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version