News
Daraja la Nyali Kufungwa Kuruhusu Ubomozi wa Jengo
Serikali ya kaunti ya Mombasa imetangaza kwamba italifunga daraja la Nyali kwa mda wa saa moja siku ya Jumatano tarehe 9 kuanzia mwendo wa mchana ili kuruhusu ubomozi wa jengo lililojengwa karibu na hospitali kuu ya ukanda wa Pwani mjini Mombasa.
Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na kutiwa saini na Gavana wa Mombasa Abdulswamad Sharrif Nassir, wanaotumia barabara ya Nyali-Mombasa wameagiza kuvuka daraja hilo kabla ya saa moja na nusu asubuhi.
Taarifa hiyo imewataka wakaazi walio karibu na jengo hilo kukaa umbali wa kilomita 1.2 ili kuepuka madhara huku wagonjwa katika hospitali ya ukanda wa Pwani wakihamishiwa maeneo salama kwani ubomozi huo umethitishwa kwamba utatumia vilipuzi.
Hata hivyo Serikali ya kaunti ya Mombasa, maafisa wa idara ya ulinzi nchini KDF, pamoja na wale wa kukabiliana na majanga wamewataka wakaazi kuwa watulivu wakati ubomozi huo ukiendelea.