Sports

Timu Ya Taifa Ya Nigeria Super Falcons Imepokea Zawadi Nono Kutoka Kwa Rais

Published

on

 Mabingwa wa Bara Afrika kwa soka la akina dada Super Falcons wamevuna vinono kutoka kwa rais wa taifa hilo punde tu baada ya kutua kutoka mjini Rabat Morocco.
Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu akitangaza zawadi zifuatazo kwa timu ya Super Falcons:
Kila mchezaji atapokea dola 100,000 za Kimarekani
Kila mchezaji atapewa nyumba ya vyumba vitatu
Kila mwanachama wa benchi la ufundi atapokea dola 50,000 za Kimarekani
Zaidi ya hayo, Jukwaa la Magavana wa Nigeria limewazawadia kila mchezaji kiasi cha ₦10 milioni (takriban dola 6,000 za Kimarekani).
Vipusa hao waliwashinda wenzao wa Morocco magoli 3-2 kwenye fainali kali iliosakatwa siku ya Jumamosi na kutwa ubingwa huo likiwa ni taji lao la kumi katika historia ya kombe hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version