News
Cheruiyot: Tutaidhinisha Majina ya Makamishna wa IEBC Bungeni
Wabunge wanaoegemea mrengo wa Kenya Kwanza wameapa kuidhinisha orodha ya makamishna pamoja na Mweneyekiti wa Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC punde tu itakapowasilishwa bungeni.
Wabunge hao wameshauri viongozi wanaopinga orodha hiyo kutafuta mbinu tofauti ya kuipinga.
Wakiongozwa na Kiongozi wa walio wengi katika bunge la Seneti ambaye pia ni Seneta wa Kericho Aaron Cheruiyot, viongozi hao wamedai kwamba Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka alihusishwa katika uundaji wa sheria za uchaguzi za Tume ya IEBC na uteuzi wa jopo la uchaguzi.
Wakati huo huo viongozi hao wamedai kushangazwa na Kalonzo kwa kutokuwa mwaminifu baada ya kutangaza kutounga mkono orodha ya waliyopendekezwa kushikilia nyadhfa katika Tume ya IEBC.