Wafanyibiashara wa mitumba eneo la Diani wafunga biashara zao

Wafanyibiashara wa mitumba eneo la Diani wafunga biashara zao

Wafanyibiashara wa mitumba katika soko la Diani, kaunti ya Kwale, wamelazimika kufunga biashara zao kutokana na kudorora kwa shughuli za kibiashara katika kipindi hiki cha msimu wa watalii wachache na mvua zinazoendelea kushuhudiwa katika eneo hilo.

Wafanyabiashara hao wanasema idadi ya wanunuzi imepungua kwa kiasi kikubwa, hali iliyosababisha nguo nyingi kukosa soko.

Kulingana na wafanyibiashara hao wanategemea zaidi watalii wa ndani na nje  na kutokana na msimu huu kuwa uko uko chini wateja wamepungua hali inayofanya maisha kuwa mgumu.

Wanasema  wamelazimika kutupa baadhi ya nguo kwani  zimesalia sokoni kwa  muda mrefu hadi zingingine kuharibika, jambo ambalo limepelekea kupata hasara kubwa.

Aidha, wameongeza kuwa bei ya nguo za mitumba imeendelea kupanda ambapo wananunua ngunia moja kwa shilingi elfu 40 huku mauzo yakizidi kushuka.

“ Biashara imedorora sai kwani hakuna wateja ikizingatiwa kuwa tunategemea sana watalii na sasa hakuna wageni hata imetulazimu kutupa nguo kwani ngigi zimeharibika baada ya kukaa kwa mda mrefu bila kununuliwa”.

Taarifa ya Pauline Mwango