Ujenzi wa daraja la Mwachande latoa matumaini ya miaka kwa wakaazi

Ujenzi wa daraja la Mwachande latoa matumaini ya miaka kwa wakaazi

Kwa miaka mingi, wakaazi wanaotumia kivuka cha Mto Ramisi eneo la Mwachande kaunti ya Kwale, wamekabiliwa na changamoto wanapotafuta njia za kufuka daraja hilo dogo linalounganisha Msambweni na Lunga Lunga.

Wakati wa msimu wa mvua, wakaazi wanasema kivuko cha zamani ilikuwa vigumu zaidi kutumia na wakati mwingine kuwa hatari jambo lililokatiza safari za kwenda sokoni, shuleni, vituo vya afya na maeneo ya kazi.

Ujenzi wa Daraja la Mwachande umebadilisha hali hiyo na kuleta matumaini ya usafiri salama pamoja na kuimarika kwa shughuli za kiuchumi katika eneo hilo.

Daraja hilo linalojengwa na Mamlaka ya Barabara za mitaa (KeRRA) pamoja na barabara ya Milalani–Kikoneni–Mwangulu, kwa gharama inayokadiriwa kuwa shilingi milioni 538 inalenga kusahisisha shughuli za usafriki.

Kulingana na Mwanamisi Mwaruma, umuhimu wa mradi huu haupimwi kwa saruji na maelezo ya uhandisi, bali kwa kuhakikisha usafiri rahisi, akisema wakaazi wamevumilia miaka mingi na changamoto nyingi lakini ujenzi wa daraja hilo utarahisha shughuli za uchukuzi.

“Kwetu, tofauti kubwa zaidi ni kwamba usafiri utakuwa rahisi sasa. Tumeteseka hapa kwa miaka mingi, hasa wakati wa mvua,” alisema Mwaruma.

Wakaazi wa Mwachenda wapongeza ujenzi wa daraja la Mwachenda katika mtu Ramisi

Kwa upande wake mkaazi wa eneo hilo Suleiman Muhammed, alisema maendeleo ya mradi huo yanawakilisha kutimizwa kwa ombi la muda mrefu la jamii.

“Tumelisubiri daraja hili kwa muda mrefu sana. Kinachotuhusu ni kuona kazi hatimaye ikiendelea na kujua kwamba watu wataweza kuvuka kwa usalama,” aalisema Suleiman.

Baadhi ya wakaazi waliepongeza utawala wa Rais William Ruto kwa kusukuma mradi huo kuelekea kukamilika, wakisema wanatumaini kuwa muunganiko huo ulioboreshwa utaongeza biashara, kupunguza changamoto za usafiri na kurahisisha familia kufikia huduma muhimu.

Kwa wakazi wa Mwachande, manufaa hayo yanatarajiwa kuwa ya moja kwa moja — vivuko salama zaidi, safari fupi, urahisi wa kusafirisha mazao ya kilimo, upatikanaji bora wa masoko na kupungua kwa usumbufu wakati wa mvua kubwa.

Taarifa ya Mwanahabari wetu