News
Bi Rachel: Serikali itahakikisha kila mmoja anawezeshwa kiuchumi
Mama wa Taifa Rachel Ruto amesema serikali kuu inaendeleza mikakati thabiti kuhakikisha kila mmoja hapa nchini anawezeshwa vilivyo wakiwemo wajane ili waweze kujiendeleza kimaisha.
Mama wa Taifa alihakikisha kujitolea kikamilifu kwa serikali kuu kuwawezesha wajane kote nchini, akisisitiza kumujuishwa kwao na wala sio kuwatenga kama inavyofanya kwa watu wengine wakiwemo walio na uatilifu.
Mama wa Taifa pia aliwataka vijana, wajane na watu walio na uatilifu nchini kuhakikisha wanachukua mikopo kwenye hazina ya Hustler ili wazitumie katika kuanzisha barabara mbalimbali ambazo zitawasaidia kupata mapato ambayo yatawawezesha kukidhi mahitaji yao na ya familia.
Aidha aliwahimiza kujiunga na vikundi ili kunufaika na hazina zilizopo za kiuchumi ambazo zimeanzishwa na serikali kuanzia viwango vya wadi hadi kitaifa.
“Ni vizuri kina mama tuweze kuingia katika vikundi, ili vikundi hivi viweze kuwahudumia. Serikali ina mipango mingi ambayo inaweza kusaidia akina mama. Tuingie vikundi na tusivunje vikundi,” alisema Mama Taifa.
Taarifa ya Janet Mumbi