Business
Bei ya Madaktari wa Kibinafsi Yawasukuma Wafugaji Kwenye Hasara
Wakulima katika eneo la malindi kaunti ya Kilifi wanaiomba serikali ya kaunti kuajiri madaktari zaidi wa mifugo ili kuboresha sekta ya ufugaji kwani wafugaji wa mashinani wamekuwa wakitegemea madaktari binafsi ambao hutibu mifugo wao kwa bei ghali.
Wakiongozwa na Nzaro Mlewa, wafugaji hao wanasema wamekuwa wakipitia changamoto ya huduma za matibabu kwa mifugo wao hali inayoathiri pakubwa sekta ya ufugaji eneo hilo.
Aidha Mlewa amedai kuwa wakulima kutoka mashinani wanakadiria hasara kutokana na mifugo yao kushambuliwa na maradhi huku wakishindwa kupata madakitari .
Sasa wanaitaka serikali ya kaunti kuajiri madakitari zaidi ili kuwapunguzia changamoto na hasara wanazopitia.
“Serikali inapaswa kuajiri madakitari wa mifugo zaidi ili tusaidia sisi wakulima wa mashini kwa sababu mara nyingi imetulazimu kutafuta madakitari wa kibinafsi ilihali wengi wetu hatuna uwezo maana wako ghali.”