Sports
Alcaraz,Sabalenka ndaani ya Robo Fainali,Wimbledon
Bingwa mtetezi wa Wimbledon na mchezaji anayeorodhshwa wa pili ulimwneguni kwa sasa mchezo wa Tennis Carlos Alcaraz raia wa Uhispania pamoja na Aryna Sabalenka anayeotodhshwa wa kwanza upande wa akina dada wamejitosa katika robo fainali mashindano ya Wimbledon Uingereza.
Alcaraz sasa atamenyana na Cameron Norris raia wa Uingereza akitarajiwa kuingia kwenye daftari za kumbukumbu kwa kuwa miongoni mwa wachezaji ambao wameshinda msururu huo kwa miaka mitatu mfululizo wengine ambao wamewahi kushinda mara tatu kwa mpigo ni pamoja na;Bjorn Borg, Pete Sampras, Roger Federer and Novak Djokovic.
Kwa upande wake nyota wa upande wa akina Aryna Sabalenka baada ya kushinda mechi zake zote sasa ameratibiwa kumenyana na Laura Siegemund akisaka taji la nne la Grand Slam kule Wimbledon.