News
Trent Arnold Aondoka Anfield
Beki wa taifa la Uingereza Alexander Trent Arnold ametangaza kugura kilabu ya Liverpool baada ya msimu huu kukamilika. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ametangaza kugura kilabu hiyo baada ya kuhudumia kwa zaidi ya miaka 20 akitokea kwenye akademia ya The Reds.
kwenye kanda aliyopost kwenye mitandao yake ya kijamii beki huyo wa kulia ameshukuru kilabu hio na mashabiki wake kwa nafasi na ungwaji mkono ambao walimpa tangu akiwa mchezaji mdogo kilabuni humo.
TAA amefanikiwa kufunga magoli 18 na kuwa beki aliyechangia kupiga basi nyingi epl akiwa amepakua pasi 64 kwa wenzake kufunga,akiwa ameshinda mataji 2 ya Epl moja ya kilabu bingwa ulaya miongoni mwa mataji mengine.
Inaaminika mchezaji huyo tayari amekubaliana na uhamisho wa bila malipo na kilabu ya Real Madrid baada ya kudinda kutia wino mkataba mpya na The Reds akiwa tayari amekubaliana na matakwa yake binafsi.