News

Rising Stars Yapigwa Na Morocco Afcon

Published

on

Timu ya soka vijana wasiozidi umri wa miaka 20 Rising stars wameanza vibaya kampeini ya Afcon kwa kupoteza pembamba magoli 3-2 dhidi ya Morocco mechi ya ufunguzi jana usiku ugani 30th June stadium mjini Cairo Misri.

Vijana wa kocha Salim Babu walichukua uongozi wa mapema kupitia mshambulizi Lawrence Ouma dakika ya 16 kabila ya Yasiri Sabiri kuwasawazishia Morocco dakika 45 na badaye kuongeza la pili dakika ya 55.

Mshambulizi Hassan Beja aliweka mambo sawa dakika ya 71 baada ya pasi safi kutoka kwa Aldrine Kibet ila Morocco walikua jambo lao Reda Lalooi akifunga la tatu dakika ya 78.

katika mechi nyingine kundi Ba Nigeria 1-0 Tunisia,Rising stars watashuka uwanjani kucheza na Tunisia mechi ya pili Mei 7.

Hii leo;Senegal vs Central Africa

Dr.Congo vs Ghana .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version