News
Jopo la ushauri na Maimamu eneo la Takaungu lasisitiza Samuel Charo alisilimu kwa hiari yake
Jopo la ushauri na maimamu katika eneo la Takaungu wadi ya mnarani kaunti ya Kilifi limepinga madai yalioibuliwa na wanafamilia wa kijana aliyeuawa baada ya kumuua na kula matumbo ya mzee mmoja aliyekuwa ustadh aliyetambulika kama Ainen.
Kwa mujibu wa ustadh Abubakar Ratili wa masjid Answar kule Takaungu, marehemu Samuel Kirao Charo alisilimishwa na kupewa jina Zakariyah akisisitiza kuwa marehemu alisilimu kwa hiyari yake mbele ya waislam wengine kwenye msikiti huo
Aidha Sheikh Mahadh Ali ambaye pia ni imam wa msikiti Maryam eneo hilo la Takaungu pamoja na Ustadh Mohamed Khamis wameeleza kuwa dini ya kiislam inaruhusu mwili kuzikwa usiku akikashifu swala la kuhusisha hatua hiyo na ushirikina kama ilivyodaiwa na baadhi ya watu.
Jopo hilo pia limeeleza kuwa wanafamilia walihusishwa ila walidinda kushirikiana nao jambo lililopelekea jamii hiyo ya kiislamu kuendeleza maziko ya marehemu kwa mujibu wa Imani ya dini ya kiislam.