News
Gor Mahia Yailaumu Fkf Kutokana Na Vurugu Gusii
Mabingwa mara 21 ligi kuu humu nchini kilabu ya Gor Mahia imeilaumu shirikisho la soka nchini FKF pamoja na kamati inayosimamia ratiba ya mechi za ligi kuu kutokana na vurugu iliyoshuhudiwa ugani Gusii wikendi.
Kupitia barua kilabu hiyo imelaani kitendo hicho huku ikisema kwamba shirikisho pamoja na wasimamizi wa ligi hiyo waliwapuuza kutokana na ubora wa uwanja huo kuandaa mechi kubwaa kama hiyo ila wakapuuza kabisaa.
Kulingana na katibu mkuu wa kilabu ya Gor mahia Nicanor Arun ni kwamba hawatachezea tena uwanjani humo siku zijazo wakilaumu mashabiki wa Shabana kwamba ndio walianza vurugu hiyo ugani Gusii.
Katibu huyo aliendelea kusema alishangaa licha ya kamanda wa mechi hiyo kutaka mechi hiyo kuhairisha viongozi wa Shabana walisisitiza mechi iendelee kama ilivyopangwa.
Takwimu ambazo zimetolewa na maafisa wa usalama ni kwamba zaidi ya watu 72 waliweza kutibiwa baada ya kujeruhiwa kwenye vurumahi hio kogalo wakiponyoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya wapinzani wao Shabana.